Skip to main content

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIWA NA WAOMBAJI KAZI UTUMISHI WA UMMA




MASWALI NA MAJIBU YA WADAU WA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

PATA MAJIBU YA BAADHI YA MASWALI AMBAYO YAMEKUWA YAKIULIZWA NA WADAU WA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA KUPITIA NJIA MBALIMBALI ZA MAWASILIANO WAKITAKA KUPATIWA UFAFANUZI, AIDHA, TUTAENDELEA KUTOA MAJIBU KILA MARA KWA MASWALI TOFAUTI KADRI YALIVYOTUFIKIA.

1. Je, ni mambo gani napaswa kuzingatia wakati wa kuandaa wa Wasifu binafsi (CV)?
i. Juu Kabisa
Mhusika ataje majina yote rasmi anayotumia kwa herufi kubwa kama yalivyo kwenye vyeti au viapo kama vipo.
ii. Maelezo yake kwa kifupi
Matarajio yake na ofisi anayoombea kazi itegemee nini toka kwake.

iii. Historia yake ikiwemo;-
  • Miaka yake
  • Jinsia yake
  • Hali ya ndoa
  • Uraia
iv. Historia ya Elimu
Aeleze elimu aliyonayo kuanzia kiwango kikubwa cha elimu alichonacho hadi cha mwisho cha chini alichoanzia ikiwemo, Vyuo alivyosoma na mwaka aliohitimu na vyeti alivyotunukiwa kwa mfano:
  • Masters of Science in Human Resource Management – Mzumbe University 2015,
  • Bachelor Degree in Law (LLB) – University of Dar es Salaam (UDSM) 2012,
  • Advanced Certificate of Secondary Education Newala Secondary School 2003,
  • Certificate of Secondary Education Zanaki Secondary School 2000.

v. Historia ya Uzoefu wa kazi alionao
Uchambuzi huo uanzie nafasi aliyonayo na kazi ya sasa hadi aliyoanzia kushika ikionyesha Mwajiri, Kipindi/Muda na Majukumu aliyokuwa akiyatekeleza.

vi. Wadhamini na anwani zao
Majina ya wadhamini wasiopungua watatu yatajwe yakiwa na anuani kamili za barua, barua pepe, simu za mikononi na ofisi wanazofanyia kazi ili kurahisisha mawasiliano nao pindi itakapohitajika kufanya hivyo, inashauriwa wawe watu wake wa karibu wanaoweza kutoa taarifa sahihi juu yake.

vii. Kiapo/Tamko Saini na Tarehe
Mhusika aandike maneno ya kuthibitisha taarifa alizotoa ni sahihi na za kweli aweke saini yake na tarehe ya kuwasilisha wasifu wake na atawajibika nazo endapo atakuwa amepotosha.

2. Masuala yapi napaswa kuzingatia katika kuandika barua ya maombi ya kazi?
i. Anuani ya Mwombaji
  • Sanduku la Posta 
  • Mkoa/Wilaya aliyopo 
  • Tarehe
  • Barua pepe
  • Namba ya simu
ii. Anuani ya anayetangaza nafasi ya kazi
iii. Anuani ya Mwajiri (K.k......)
Kwa wale ambao barua zao inabidi kupitishwa na mwajiri lazima barua igongwe mhuri wa ofisi au wa aliyepitisha barua ikionyesha na tarehe iliyopitishwa. (Mfano: Katibu Mkuu, Katibu, Mkurugenzi Mkuu nk).
iv. Kichwa cha habari cha barua
Lazima kieleze wazi nafasi inayoombwa ikiwezekana ibainishwe pia na Taasisi inayohusika ili kuweza kuzitofautisha

v. Madhumuni ya barua
  • Mwombaji aeleze elimu aliyonayo akianzia na elimu ya juu aliyonayo na chuo alichomaliza/vyuo alivyomaliza
  • Umri wake
  • Kwa nini anaomba nafasi na uzoefu wake kwa ufupi sana
vi. Hitimisho
  • Matarajio yake (kwa kifupi)
  •  Jina
  • Kuhakikisha umeweka saini
3. Je, naweza kufahamu wajibu na vigezo ninavyopaswa kuvizingatia kama mwombaji wa nafasi za ajira kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (masharti ya jumla).

i. Kuhakikisha nafasi anayoomba imetangazwa na Sekretarieti ya Ajira ili kuthibitisha hilo mhusika ajiridhishe kwa kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz
ii. Mwombaji wa nafasi ya kazi awe ni Raia wa Tanzania.
iii. Mwombaji wa nafasi ya kazi aambatishe cheti cha kuzaliwa.
iv. Mwombaji wa nafasi ya kazi ambae tayari ni Mtumishi wa Umma na amejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na alizonazo anatakiwa apitishe barua za maombi ya nafasi za kazi kwa Mwajiri wake na Mwajiri ajiridhishe ipasavyo.
v. Mwombaji wa nafasi ya kazi anapaswa kuandika nafasi ya kazi anayoiomba na iandikwe katika kichwa cha habari cha barua.
vi. Mwombaji wa nafasi ya kazi anatakiwa kuweka anwani na namba za simu zinazopatikana pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika
vii. Vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Vyuo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

- Shahada ya juu/Shahada/Stashahada ya juu/Stashahada/Astashahada.
- Cheti cha kufaulu mtihani wa kidato cha IV na VI
- Cheti cha Kompyuta,
- vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iingizwe kwenye mfumo katika sehemu iliyoainishwa.
“Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati ya matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) huwa havikubaliki kwa kuwa sio vyeti, mhusika huruhusiwa kutumia (Academic Transcript) pale tu vyeti vya Chuo alichomaliza bado havijatolewa ila vikishakutolewa anapaswa kutumia cheti halisi.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
Ni marufuku kwa mwombaji wa fursa za ajira Serikalini kuwasilisha kwa kujua au kutokujua taarifa au sifa za kugushi maana itakapobainika mhusika atachukuliwa hatua za kisheria.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Umri uliopo Kisheria ambao unamwezesha mwombaji kuajiriwa katika utumishi wa umma kwa masharti ya kudumu ni miaka 45. Umri huu umewekwa kisheria ili kumwezesha kuchangia mafao yake ya uzeeni kwa miaka 15. Aidha, kwa wale wenye umri wa zaidi ya miaka 45 wanaweza kuajiriwa kwa mkataba kulingana na mahitaji.
Wakati wa kuwasilisha maombi yake aambatanishe nakala ya vyeti vya taaluma kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa kuzingatia sifa ya kazi husika.
Uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira hauruhusiwi, waombaji kazi wanapaswa kutumia njia ya mtandao tu kupitia www.ajira.go.tz ataona sehemu imeandikwa (Recruitment Portal) ataingia hapo kwa kufuata maelekezo hatua kwa hatua.
xiv. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE) kabla ya kuviwasilisha Sekretarieti ya Ajira.

4. Je, Mwombaji wa nafasi ya kazi anatakiwa kutekeleza vitu gani kabla ya kuwasilisha maombi ya kazi kwenye Mfumo wa Sekretarieti ya Ajira?

i. Mwombaji awe ameona tangazo la nafasi ya kazi na kulisoma, kulielewa kabla ya kuwasilisha maombi ya kazi.

ii. Mwombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoomba katika barua yake ya maombi ya kazi.

iii. Mwombaji awe amejisajili kwenye mfumo wa maombi ya kazi (recruitment portal) http://portal.ajira.go.tz

iv. Mwombajianapaswakuambatishanyarakazakemuhimukulinganana tangazo la nafasi ya kazi.

v. Mwombaji kazi kuhakikisha ameingiza cheti cha kuzaliwa na vyeti vyake vya elimu kwa ngazi mbalimbali ambavyo vimehakikiwa na kupigwa muhuri na Mwanasheria kulingana na tangazo la nafasi za kazi linavyomtaka.

vi. Mwombaji kazi ambae amesoma ngazi ya cheti (Astashahada), pia ana cheti cha diploma (Stashahada) na pia ana cheti Stashahada ya juu ambayo ni (Advanced Diploma) au cheti cha (Shahada yaani Degree ya kwanza) ajue yeye anaruhusiwa kuomba kazi ya Degree tu itakapotangazwa kulingana na fani yake. Akiomba kazi ya Astashahada, au Stashahada mfumo utamkatalia, kwakuwa kazi hizo ni kwa ajili yawe ambao elimu waliyonayo kwa wakati husika ni ngazi hiyo tu na si vinginevyo.

vii. Baada ya kukamilisha kujaza taarifa zako katika mfumo wa maombi unapaswa kupakia nyaraka stahiki zilizoainishwa baada ya hapo mfumo utakujulisha papo hapo kupokelewa au kukwama kwa maombi yako.

Aidha, endapo mstahiliwa ana changamoto ya kitaalamu yaani inayohusiana na mfumo anaweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0735-398259 na endapo ni suala la malalamiko anatakiwa kuwasiliana nasi kwa namba 0736-005511.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Sekretarieti ya Ajira

Comments

Popular posts from this blog

NAFASI ZA KAZI MPYA UNICEF (Re- Advertisement): Temporary Appointment - Health (Financing) Specialist P3 Tanzania

APPLY NOW Job no:   576667 Contract type:   Temporary Appointment 💥 TAZAMA NAFASI MPYA UNICEF SENIOR OPERATIONS ASSOCIATIONS Duty Station:   Dar-es-Salaam Level:   P-3 Location:   United Republic of Tanzania Categories:   Health Deadline: 10 Nov 2024 11:55 PM UNICEF works in over 190 countries and territories to save children’s lives, defend their rights, and help them fulfill their potential, from early childhood through adolescence. At UNICEF, we are committed, passionate, and proud of what we do. Promoting the rights of every child is not just a job – it is a calling. UNICEF is a place where careers are built: we offer our staff diverse opportunities for personal and professional development that will help them develop a fulfilling career while delivering on a rewarding mission. We pride ourselves on a culture that helps staff thrive, coupled with an attractive compensation and benefits package. Visit  our website  to learn more about what we ...

Nafasi za Kazi Mpya UNICEF-Senior Operations Associate, GS7, Zanzibar, Tanzania.

To Apply Click Here>>> APPLY NOW The UNICEF Tanzania office is seeking to recruit a Senior Operation Associate based in Zanzibar.  The successful candidate will be responsible for the operations functions, facilitate change, provide risk informed, solution-focused analysis, advice and services and contribute to programme and management decisions for delivering results for children in specific operational contexts. Location:   United Republic of Tanzania Deadline:   13 Nov 2024 11:55 PM Job no:   576754 Contract type:   Fixed Term Appointment Duty Station:   Zanzibar Level:   G-7 Categories:   Administration UNICEF works in over 190 countries and territories to save children’s lives, defend their rights, and help them fulfill their potential, from early childhood through adolescence. At UNICEF, we are committed, passionate, and proud of what we do. Promoting the rights of every child is not just a job – it is a calling. UNICEF is a place w...

VARIOUS JOBS OPPORTUNITIES TANZANIA TODAY

NEW JOBS VACANCIES: Program Monitoring and Evaluation Officer-Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) https://wildlifetanganyika.blogspot.com/2024/11/program-monitoring-and-evaluation.html NEW JOBS POSITIONS: Senior Technical Advisor – Family Planning Services at Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) https://wildlifetanganyika.blogspot.com/2024/11/new-jobs-positions-senior-technical.html 14 Various Jobs Positions: Mbeya University Of Science And Technology(MUST) https://wildlifetanganyika.blogspot.com/2024/11/14-various-jobs-positions-mbeya.html NEW VACANCIES: SECP Grants and M&E Officer at Frankfurt Zoological Society https://wildlifetanganyika.blogspot.com/2024/11/new-vacancies-secp-grants-and-m-officer.html