Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mafia anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi moja (1) ya Mtendaji wa Kijiji.
1. SIFA ZA MWOMBAJI
Mhitimu wa Kidato cha Nne / Sita wenye Cheti/ Stashahada NTA Level 5 katika moja ya fani zifuatazo:
- Utawala
- Maendeleo ya Jamii
- Usimamizi wa Fedha
- Sayansi ya Sanaa na Sheria.
Wawe wamesoma vyuo vinavyotambulika na Serikali.
2. MSHAHARA
Mshahara unaanza na Ngazi ya TGS B.
3. MAJUKUMU YA KAZI
i. Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
ii. Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na
msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji;
iii. Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya Maendeleo ya
kijiji;
iv. Kuratibu mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
v. Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na taratibu za uendeshaji wa Serikali ya
Kijiji;
vi. Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha
wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini,
na kuongeza uzalishaji mali;
vii. Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalamu katika Kijiji;
viii. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
ix. Mwenyekiti wa Kikao cha wataalamu waliopo katika Kijiji;
x. Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
xi. Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji; pamoja na
xii. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

Comments
Post a Comment