Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kupitia Kibali cha Ajira Mbadala kwa Watendaji wa Vijiji, Kibali chenye Kumb. Na. FA 170/358/01’B’/92 cha tarehe 07 Agosti, 2020 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais. Mkurugenzi Mtendaji anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kuomba kazi ili kujaza nafasi za kazi ya AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III.
1.0 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III - NAFASI 02
1.1 SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa awe na cheti cha kufaulu Kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) na waliohitimu mafunzo ya Cheti (Astashahada) katika fani zifuatazo: Utawala, Uongozi na Usimamizi wa Fedha, Sheria, Elimu ya Jamii, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
1.2 KAZI NA MAJUKUMU
i. Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
ii. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji.
iii. Kiongozi wa wataalam (watumishi wa serikali) katika kijiji.
iv. Mhasibu (Afisa masuuli) na Mtendaji Mkuu wa kazi za kila siku za Serikali ya
Kijiji.
v. Kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Taratibu zinazotolewa na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
vi. Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na
Msimamizi wa utawala bora katika kijiji.
vii. Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
viii. Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya
Kijiji.
ix. Kutekeleza shughuli nyingine atakazopangiwa na Mwajiri.
x. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
1.3. MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B

Comments
Post a Comment