Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Tamasha la Zuchu Zanzibar Kuleta Mapinduzi Zenjifleva



MSANII wa Muziki Zuhura othman a.k.a Zuchu amefunguka sababu ya kufanya show yake kubwa visiwani Zanzibar huku akiwataka wasanii wa Zanzibar kuunga Mkono Show hiyo.

Waziri wa habari ,vijana ,utamaduni na Michezo Tabia Mwita amempongeza Zuchu kwa kuona ipo haja ya Kusaidia wasanii wa kizanzibar kunyanyuka kisanaa hasa Muziki .

"Nipo kwa ajili ya kuunga Mkono idea ya Zuchu kuonyesha kwa jinsi gani wasanii wa zenjifleva wananyanyuka na kupata nafasi ya kufika mbali kupitia Muziki ni jambo la kipekee na lenye mlengo wa kukuza Sanaa yetu upande wa Zanzibar."

Hata hivyo Mwita ameeleza kuwa upande wazanzibar wapo wasanii wengi lakini Kuna Mambo machache ambayo yamekua yakiwakwamisha kutofika mbali au wengine kutokufika wanapotaka na hatimae kukata tamaa ya kuendelea kimuziki.




"Zuchu alikuja na Hilo wazo hivyo nikamuhaidi kuunga Mkono na nimekuja kuonyesha support katika wizara yangu ya habari na Michezo kuonyesha kwa kiasi gani Jambo hili nimewiwa kulibeba tumeona anafanya vizuri kwa Sasa hivyo namuamini Jambo hili atalibeba na sisi Kama wizara tutaliunga Mkono asilimia zote ".

Naomba nitoe wito kwa wasanii kushirikiana na Msanii Zuchu kuhakikisha wasanii wa zenjifleva wanafika mbali na pia amepongeza uongozi wa Wasafi (WCB) kuona ipo haja ya Kusaidia wasanii wa Zanzibar.

Kwa upande wake Zuchu ambae ni Balozi Kampuni ya m zantel amepongeza Sana Kampuni hiyo kwa kumpa ushirikiano na kuwasilisha wazo na kuona kwa jinsi gani wanalibeba na Kusaidia wazanzibar kwani mkataa kwao mtumwa.

"Nimefanya vizuri nje na ndani ya nchi nimeona kwa Sasa nisiende Mikoa mengine nianze nyumbani ndio maana Tamasha hili tumelipa jina la "Zuchu coming how" ni mahususi kwa ajili ya Wasanii wa zenjifleva hivyo nategemea watajitokeza wasanii wengi wasasa na wale wa zamani ili kutimiza haja zao kwani wapo wenye kutamani kutoa soko la Muziki kimataifa na hawakufanikiwa kufika hivyo kupitia tamasha hili wataweza kukutana na watayarishaji wa Muziki na Mapromota mbalimbali."

Zuchu amesema huko mwanzo havikuwahi kufanyika hivyo kwa Sasa wameamua kwa pamoja kukuza Muziki wa Zanzibar.

"Hii nibahati ya dhahabu hivyo matarajio yangu kuona tunakwenda kwenye anga nyingine na kuleta Mapinduzi hasa ya kimuziki."

Hata hivyo Zuchu amesema kupitia tamasha linalotarajiwa kuanza agosti 21katika viwanja vya amani visiwani Zanzibar mwaka huu wasanii watapata fursa nyingi kwa namna gani wanatoboa kimuziki.

"tutaendesha programu mbalimbali za kimuziki kuanzia julai 24 mwaka huu kwa ajili ya kutoa programu mbalimbali na nimekua na shahuku kubwa ya Kusaidia nyumbani nimesema nirudi nyumbani Kwanza.

Pia ameeleza sababu ya "Zuchu home coming" kuwa angependa kushiriki na wasanii asilimia kubwa kwani uwezo wanao na Nia wanayo.

Hata hivyo Zuchu ametaja Tamasha Hilo litapambwa na Ngoma mbalimbali,vidumbaki na taarab za zamani na sasa na kutakua na wasanii mbalimbali kutoka bara ili kuweka umoja wetu lakini hasa hasa wazanzibar".