Hot Posts

6/recent/ticker-posts

TANZIA: Anna Mghwira Afariki Dunia (62)| Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mstaafu



Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, na mgombea urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Mama Anna Elisha Mghwira, amefariki dunia leo tarehe 22July 2021 akiwa na umri wa miaka 62, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha, majira ya mchana, ambapo taarifa zinadai kwamba takribani siku saba zilizopita alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua ambapo baadaye hali yake kuwa mbaya alihamishiwa hospitali ya Mount Meru.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!.