Wanafunzi 4,105 wamechaguliwa kujiunga kidato cha tano kwa mwaka huu katika uchaguzi wa awamu ya pili kutokana na waliochaguliwa awamu ya kwanza kutoripoti kwenye shule walizopangiwa. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Prof.Riziki Shemdoe, wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma. Prof. Shemdoe amesema kuwa kati ya wanafunzi waliochaguliwa, wanafunzi 499 (wavulana 424 na wasichana 75) wamepangiwa tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 3,604 wakiwemo wavulana 3,461 na wasichana 143 wamepangiwa tahasusi za masomo ya Sanaa na Biashara. Amebainisha kuwa upangaji wa awamu ya pili umefanyika baada ya Wizara kujiridhisha na nafasi zilizo wazi katika shule ambazo wanafunzi hawakuripoti. “ Kwa kuangalia idadi ya wasichana waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili imekuwa ndogo, hii ni kwa sababu katika uchaguzi wa awamu ya kwanza wanafunzi wote wasi...
Your First Step Towards Success