Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Tundu Lissu na wenzake wafutiwa kesi iliyokuwa inawakabili

 


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifuta kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao (Chadema) Tanzania Bara, Tundu Lissu na wenzake watatu.


Ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.