Skip to main content

Mfahamu Mtanzania Abdulrazak Gurnah Aliyeshinda Tuzo ya Nobel ya Fasihi 2021



 Raia wa Tanzania Abdulrazak Gurnah ndiye mshindi mpya

Akimtangaza kuwa mshindi siku ya Alhamisi , kituo kinachotoa tuzo hizo kilimpongeza Gurnah kwa kuangazia suala la ukoloni na athari zake katika utunzi wake.

Tuzo hiyo inayotolewa na kituo hicho cha Sweden ina thamani ya $1.14m au £840,000.


Gurnah mwenye umri wa miaka 73 ni mwandishi wa riwaya 10 , ikiwemo Paradise na Desertion.


'Tamaduni na mabara'

"Kujitolea kwa Abdulrazak Gurnah katika kuangazia ukweli na masuala mengine kwa urahisi bila kuchukiza kunashangaza'' , ilisema kamati ya tuzo ya Nobel kuhusu fasihi katika taarifa yao.

"Riwaya zake zimetungwa kufuta maelezo ya uwongo na kuyafungua macho yetu kwa Afrika Mashariki iliojaa tamaduni tofauti ambazo hazijulikani katika sehemu nyengine za ulimwengu."

"Wahusika [wake] hujikuta katika hali ya kutatanisha kati ya tamaduni na mabara, kati ya maisha ya awali na maisha yanayoibuka; ni hali isiyoweza kutatuliwa kamwe."


Akiwa mzaliwa wa Zanzibar mwaka 1948, Gurnah aliwawasili nchini Uingereza akiwa mkimbizi mwisho wa miaka ya sitini.

Alikuwa profesa wa riwaya za Kiingereza na riwaya za baada ya ukoloni katika chuo kikuu cha Kent , Cantebury hadi alipostaafu hivi karibuni.

Gurnah ni Mwafrika wa kwanza mweusi kushinda tuzo hiyo tangu Wole Soyinka . Katika mahojiano 2016 , alipoulizwa iwapo angejiita mwandishi wa riwaya za baada ya ukolini au riwaya za dunia, Gurnah alijibu : nisingetumia maneno haya nisingependa kujiita mwandishi wa aina yoyote.

Ukweli ni kwamba sidhani kama ningejiita jina jingine lolote zaidi ya jina langu. Nadhani iwapo mtu angeniuliza , ingekuwa njia nyengine ya kusema , Je wewe ni mmoja kati ya haya..? Kwa kweli ningesema hapana!. Nisingependelea kuwa na jina zaidi.

Tuzo za Nobel , ambazo zimetuzwa tangu 1901 , zinatambua ufanisi katika fasihi , sayansi , amani na uchumi.

Washindi wa awali wanashirikisha waandishi wa Riwaya kama vile Ernest Hemingway, Gabriel Garcia Marquez na Toni Morrison, washairi kama vile Pablo Neruda, Joseph Brodsky na Rabindranath Tagore, na waandishi wa michezo ya kuigiza akiwemo Harold Pinter na Eugene O'Neill.

Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani nchini Uingereza Winston Churchill alishinda kwa kumbukizi yake , Bertrand Russell kwa filosofia yake na Bob Dylan kwa mishororo yake .

Tuzo ya mwaka uliopita ilichukuliwa na mshairi wa Marekani Louise Gluck.


Comments

Popular posts from this blog

NAFASI ZA KAZI MPYA UNICEF (Re- Advertisement): Temporary Appointment - Health (Financing) Specialist P3 Tanzania

APPLY NOW Job no:   576667 Contract type:   Temporary Appointment 💥 TAZAMA NAFASI MPYA UNICEF SENIOR OPERATIONS ASSOCIATIONS Duty Station:   Dar-es-Salaam Level:   P-3 Location:   United Republic of Tanzania Categories:   Health Deadline: 10 Nov 2024 11:55 PM UNICEF works in over 190 countries and territories to save children’s lives, defend their rights, and help them fulfill their potential, from early childhood through adolescence. At UNICEF, we are committed, passionate, and proud of what we do. Promoting the rights of every child is not just a job – it is a calling. UNICEF is a place where careers are built: we offer our staff diverse opportunities for personal and professional development that will help them develop a fulfilling career while delivering on a rewarding mission. We pride ourselves on a culture that helps staff thrive, coupled with an attractive compensation and benefits package. Visit  our website  to learn more about what we ...

Tangazo la Nafasi Za Kazi Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

  Apply Now Apply Now/Omba sasa nafasi hizi za kazi

Tech-Driven Conservation: Protecting the Congo Basin Rainforest

The Congo Basin rainforest, the world’s second-largest tropical forest, plays a crucial role in global biodiversity and climate regulation.  Spanning over 500 million acres, it is home to diverse wildlife, including gorillas, forest elephants, and rare plant species.  Additionally, the rainforest acts as a major carbon sink, helping mitigate climate change. However, illegal logging, mining, and agricultural expansion pose significant threats to this fragile ecosystem. Technology is emerging as a powerful tool in the fight against deforestation and habitat destruction.  Advanced satellite imagery and AI-powered monitoring systems are being used to track illegal activities in real time, allowing conservationists to respond swiftly to environmental threats.  Drones are also being deployed for aerial surveillance, capturing high-resolution images to assess forest health and detect deforestation hotspots. Blockchain technology is revolutionizing supply chain transparency,...