Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Norway Yaondoa Vizuizi Vya Kupambana na Korona



Norway imesema inaondoa vizuizi vyote vya kupambana na janga la COVID 19, kwa sababu haioni kitisho kikubwa cha afya kwa raia wake kutokana na janga hilo, licha ya kwamba kirusi cha Omicron bado kinasambaa nchini humo. 
Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Stoere amesema huu ni muda waliousubiri kwa muda mrefu huku akisema raia wake wanalindwa vyema kwa chanjo ya COVID 19. 

Ameongeza kuwa idadi ya watu wanaolazwa hospitali wakiugua corona imepungua licha ya kusambaa kwa kirusi hicho kipya.

Kuanzia leo raia wa Norway hawatolazimika kuvalia barakoa katika maeneo yaliyojaa watu pamoja na kuondoa masharti ya kukaa umbali wa mtu na mtu. 

Kukaa karantini kwa muda wa siku 14 kumeondolewa na sasa watu wazima watakaoathirika watalazimika kukaa nyumbani siku nne tu.