Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Viboko Wauwawe




Katibu Mkuu wa Chama cha mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo, ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara yake ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuanza kuwaua Viboko, wanaoonekana kutoka ndani ya Ziwa Victoria na kwenda kurandaranda kwenye makazi ya watu na kufanya mauaji.

"Lakini ninyi wananchi msianze kuwavuna (kuwaua) viboko bila kibali, siku mkiwavuna mniambie na mimi babu yenu nije kuonja nyama yake, nasikia wana nyama tamu sana, siyo," amesema Katibu huyo wa CCM Daniel Chongolo