Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Rais Samia amteua Mwana FA kuwa naibu waziri wa michezo na utamaduni



Rais Samia Suluhu Hassan amemteua mwanamuziki Hamisi Mwinjuma almaarufu Mwana FA kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katika mabadiliko yaliyotangazwa Jumapili Februari 26, na Katibu Mkuu, Dk Moses Kusiluka, Mwana FA anachukua nafasi ya Pauline Gekul, ambaye ameteuliwa kuwa naibu waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria.

Mwinjuma ambaye ni mbunge wa jimbo la Muheza ana shahada ya uzamili ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Coventry, Uingereza.