Hello ndugu wasomaji wangu wa blogu yetu pendwa ya lusaku.com ambayo hapa huwa nashare fursa mbalimbali za kimasomo nje ya nchi na kazi hapa nchini Tanzania na Africa mashariki.
Leo nimeona nikusogezee makala itakayoelezea fursa ya jinsi ya kuagiza bidhaa kutoka China kuja Tanzania.
Awali ya yote Mimi mwandishi ninao uzoefu wa kutosha kwenye hili kwani nilifanikiwa kuenda China kimasomo mnamo mwaka 2018 Hadi 2020 ambapo nilipofika China sio kwamba nilibase kwenye masomo pekee bali nilikuwa mtu wa kujichanganya sehemu mbalimbali katika kusaka fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi kama mtanzania.
Hivyo basi Leo nitakufundisha jinsi, njia au mbinu ambazo utatakiwa kuzitumia ili uweze na wewe kufanya biashara ya kitu chochote kuagiza kutoka China kama wengine wanavyoweza kufanya hivyo mfano wafanyabiashara wengi wa kariakoo kama vanjabei, na wengine wengi wanachukua mizigo kutoka nje haswa China ingawa Kuna wengine wanachukua nchi tofauti kama uturuki, Dubai ,India n.k.
Zifuatazo ni njia za jinsi ya kufanya biashara ya kuagiza bidhaa kutoka China:-
1. Aina ya bidhaa unayotaka kununua kutoka China.
Hii inaweza kuonekana ni kawaida lakini ni muhimu kwa sababu itakusaidia kujua wapi utaipata maana China Kuna masoko makubwa kama mawili Moja ndio hili tunalolifahamu wengi wetu linaitwa Guangzhou na lingine Linaitwa Yiwu, hivyo kama utahitaji kuenda mwenyewe direct kufunga mzigo basi ufahamu aina za hayo masoko na bidhaa zinazopatikana kiurahisi huko kwenye haya masoko itakurahisiahia kwa sababu haya masoko hayapo karibu karibu hivyo unahitajika kusafiri na kutumia gharama zingine ukiwa ndani ya China. Hivyo kufahamu aina ya bidhaa ni muhimu. Mfano elektronik kama simu, tv, blender utavipata Guangzhou.
2. Supplier/ manufacturer (muuzaji au kiwanda)
Hawa ndio wauzaji wenyewe wa jumla kama ni duka kubwa lililopo kule China au mtengenezaji mwenyewe ambayo ni nzuri zaidi. Hii ni point muhimu sana kujua na ukiwa na contacts kadhaa za wauzaji waaminifu kutoka China , utaepuka gharama za kuenda mwenyewe China na utakachotakiwa kufanya ni kumtumia pesa huyo muuzaji mfano supplier wa simu smart phones ambayo yupo Guangzhou utamtumia pesa then atakufungia mzigo na kukutumia. Kwenye point zifuatazo naelezea jinsi ya kutuma mzigo na kufanya malipo ya mzigo wako.
3. WeChat App (Njia kuu ya mawasiliano China)
Hii nayo ni muhimu mno kuwa nayo, kwa sababu hakuna njia nyingine ambayo ni rahisi kama WeChat , hapa utaweza kuwasiliana na supplier wako Moja kwa Moja wakati wowote kwa lugha ya kiingereza na akakuelewa bila shida yoyote kwani WeChat App Ina uwezo wa kutafsiri meseji zote utakazo kuwa unamtumia supplier wako, pia nilisema unaweza kulipia mzigo wako ukiwa hapa hapa Tanzania, yes, Kuna kitu kinaitwa WeChat pay ambapo utaweza kuweka pesa zako kwenye WeChat wallet na ukafanya transaction za pesa hata kama haupo China au hii ikiwa ni ngumu basi Kuna bank transfer ambapo utaweza kumtumia pesa, hakikisha umejirudhisha na supplier wako kwa kuuliza watu mbalimbali ambao wameshawahi kununua bidhaa kutoka kwa huyo muuzaji na kwamba ni muaminifu, hiyo itakusaidia kutopoteza mzigo wako muda na pesa.
4. Agent wa kusafirisha mizigo Yako.
Hapa napo ndio kwenyewe kwa sababu Hawa ndio Wana mchango mkubwa sana kwa kuchelewa au kuwahi kwa mizigo Yako kufika Tanzania. Hakikisha una address za kampuni yako ya usafirishaji yenye ofisi zake China mfano Guangzhou , hiyo address ndio utakayompa supplier wa mizigo uliponunua yeye ataituma mizigo kwenye hiyo shipping cargo ambao wao watakusafirishia mpaka Tanzania, itategemea umechagua mzigo wako usafirishwe kwa njia ya anga (ndege) au maji (meli). Hapa hakikisha mzigo wako supplier ameuandika jina lako vizuri kabisa pamoja na namba zako za simu kupelekea urahisi mizigo itakapofika Tanzania, pia hakikisha muuzaji anakutumia risiti ya kielektroniki ambayo utaonyesha ukienda kuchukua mzigo ukifika.
Baada ya mzigo kufika anza kuuza mzigo wako.
Kama ulikuwa na wateja ambao walikuwa wameoda mzigo, waambie mzigo umefika au kama umeagiza kwa ajili ya kuuza dukani kwako fanya matangazo , uza na agiza mwingine na mwingine. Ni rahisi sana na inawezekana kuagiza bidhaa kutoka China.
Mawasiliano yangu ya Whatsapp ni +255626101470
Ama email: lusubilokayange@gmail.com
0 Comments