Mamlaka ya Udhibiti Usafiri
Ardhini (LATRA) imefanya kikao kilichohusisha Jeshi la Polisi Kikosi cha
Usalama Barabarani na wamiliki wa mabasi ya Sauli na New Force yaliyosababisha
ajali ya tarehe 28 Machi, 2024 majira ya saa tisa na dakika arobaini na mbili
(09:42) alfajiri, ambapo magari matatu yaligongana eneo la Mashamba ya Mpunga
Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani katika barabara ya Morogoro. Kufuatia kikao
hicho, Mamlaka imewataka wasafirishaji hao kutoa maelezo kwa maandishi kabla ya
kuchukua hatua za kiudhibiti dhidi yao.
0 Comments