Skip to main content

Tangazo la Nafasi za Kazi(11) Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga


TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga anakaribisha maombi ya kazi
kwa Watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi Kumi na moja (11) za
kazi. Tangazo hili ni kutokana na Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mchanganuo wa nafasi hizo ni
kama unavyoonekana hapa chini:-
1.0 DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 08)
2.0 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
iv. Kufanya na kusambaza nyaraka mbalimbali pale inapohitajika.
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
vi. Kufanya usafi wa gari na
vii. Kazi nyingine anazopangiwa na mwajiri.
viii. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
ix. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
x. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
xi. Kufanya na kusambaza nyaraka mbalimbali pale inapohitajika.
xii. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
xiii. Kufanya usafi wa gari na
xiv. Kazi nyingine anazopangiwa na mwajiri.

2.1. SIFA ZA MWOMBAJI.
Kuajiriwa mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form Four) na Leseni ya Daraja E au C ya
uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila
kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic driving
course) yanayotolewa na chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) au chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
2.2. NGAZI YA MSHAHARA
Mshahara utalipwa kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali. TGS B
3.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 03)
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
i) Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye Regista (Incomming
 Correspondence Register),
 ii) Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence
Register),
 iii) Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers),
 iv) Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji
v) Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji,
vi) Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling
Cabinets) au Pengine yanapohifadhiwa,
vii) Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking).
 3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato
cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe amehitimu mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level
6) katika fani ya Utunziji wa Kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi
wa compyuta.
 3.3 NGAZI YA MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – C

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
i. Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18
na usiozidi miaka 45 isipokuwa wale walioko kazini Serikalini;
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya
taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
iii. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail
Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na
Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini
(Referees) watatu wa kuaminika.
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu naTaaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale
waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazihusika.
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, - Cheti cha
mtihani wa Kidato cha IV na VI,-Computer Certificate,-Vyeti vya Kitaaluma
(Professional Certificate from Respective Boards).
v. “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya
Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vi. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi;
viii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
x. Mwisho wakutuma maombi ya kazini tarehe 03 Juni, 2025.
xi. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwekwa:-
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA SUMBAWANGA
S.L.P. 187 .
xii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo;https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ('Recruitment Portal').
xiii. Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tangazo hili limetolewana :
MANGALI.U.E
MKURUGENZI WA MANISPAA
SUMBAWANGA


#nafasimpyazakazi #daresalaamjobs #newjobsopportunities #jobstanzania #newopportunities #newemploymentopportunities #hiringnow #scholarshipsopportunities #fullyfundedscholarships #fullyfunded #mabumbe #ajiraleo #ajiraportal #ajiratz #brightermonday #cvpeople #jobshunting #jobsinarusha #jobsindar #jobsinmbeya #jobsinmwanza #jobsindodoma #chinascholarships #chinascholarshipsopportunities #ajiraportaltz

Comments

Popular posts from this blog

NAFASI ZA KAZI MPYA UNICEF (Re- Advertisement): Temporary Appointment - Health (Financing) Specialist P3 Tanzania

APPLY NOW Job no:   576667 Contract type:   Temporary Appointment 💥 TAZAMA NAFASI MPYA UNICEF SENIOR OPERATIONS ASSOCIATIONS Duty Station:   Dar-es-Salaam Level:   P-3 Location:   United Republic of Tanzania Categories:   Health Deadline: 10 Nov 2024 11:55 PM UNICEF works in over 190 countries and territories to save children’s lives, defend their rights, and help them fulfill their potential, from early childhood through adolescence. At UNICEF, we are committed, passionate, and proud of what we do. Promoting the rights of every child is not just a job – it is a calling. UNICEF is a place where careers are built: we offer our staff diverse opportunities for personal and professional development that will help them develop a fulfilling career while delivering on a rewarding mission. We pride ourselves on a culture that helps staff thrive, coupled with an attractive compensation and benefits package. Visit  our website  to learn more about what we ...

Nafasi za Kazi Mpya UNICEF-Senior Operations Associate, GS7, Zanzibar, Tanzania.

To Apply Click Here>>> APPLY NOW The UNICEF Tanzania office is seeking to recruit a Senior Operation Associate based in Zanzibar.  The successful candidate will be responsible for the operations functions, facilitate change, provide risk informed, solution-focused analysis, advice and services and contribute to programme and management decisions for delivering results for children in specific operational contexts. Location:   United Republic of Tanzania Deadline:   13 Nov 2024 11:55 PM Job no:   576754 Contract type:   Fixed Term Appointment Duty Station:   Zanzibar Level:   G-7 Categories:   Administration UNICEF works in over 190 countries and territories to save children’s lives, defend their rights, and help them fulfill their potential, from early childhood through adolescence. At UNICEF, we are committed, passionate, and proud of what we do. Promoting the rights of every child is not just a job – it is a calling. UNICEF is a place w...

VARIOUS JOBS OPPORTUNITIES TANZANIA TODAY

NEW JOBS VACANCIES: Program Monitoring and Evaluation Officer-Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) https://wildlifetanganyika.blogspot.com/2024/11/program-monitoring-and-evaluation.html NEW JOBS POSITIONS: Senior Technical Advisor – Family Planning Services at Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) https://wildlifetanganyika.blogspot.com/2024/11/new-jobs-positions-senior-technical.html 14 Various Jobs Positions: Mbeya University Of Science And Technology(MUST) https://wildlifetanganyika.blogspot.com/2024/11/14-various-jobs-positions-mbeya.html NEW VACANCIES: SECP Grants and M&E Officer at Frankfurt Zoological Society https://wildlifetanganyika.blogspot.com/2024/11/new-vacancies-secp-grants-and-m-officer.html