Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa Ibara ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011 inaipa Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na majukumu yake mengine, mamlaka ya kuajiri watumishi wa Mahakama wa kada mbalimbali.
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Mahakama ya Tanzania katika Mikoa na Wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni Afisa Hesabu II - (TGS D) nafasi 2, Msaidizi wa Hesabu II - (TGS B) nafasi 4, Operata wa Kompyuta II - (TGS C) nafasi 1, Katibu Mahsusi III – (TGS B) nafasi 4, Msaidizi wa Kumbukumbu II - (TGS B) nafasi 2, Msaidizi wa Ofisi - (TGOS A) nafasi 15 na Mlinzi - (TGOS A) nafasi 16

Comments
Post a Comment