Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Rasmi Siku Ya Kiswahili Duniani Julai 7



 Mkutano mkuu wa 41 wa UNESCO umeipitisha tarehe 7 julai ya kila mwaka kuwa siku rasmi ya maadhimisho ya kiswahili Duniani.

Azimio hilo limepitishwa na nchi zote wanachama wa UNESCO bila kupingwa leo tarehe 23.11.2021 Paris nchini Ufaransa.



Hatua hii inakifanya kiswahili kuwa lugha ya kwanza Afrika kutambulika na United Nations kuwa na siku maalumu ya kuadhimishwa. Hizi ni miongoni mwa jitihada za serikali ya Tanzania katika kukuza lugha ya kiswahli na kuenzi urithi tulioachiwa na muasisi wetu wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere .