MASWALI NA MAJIBU YA WADAU WA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA PATA MAJIBU YA BAADHI YA MASWALI AMBAYO YAMEKUWA YAKIULIZWA NA WADAU WA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA KUPITIA NJIA MBALIMBALI ZA MAWASILIANO WAKITAKA KUPATIWA UFAFANUZI, AIDHA, TUTAENDELEA KUTOA MAJIBU KILA MARA KWA MASWALI TOFAUTI KADRI YALIVYOTUFIKIA. 1. Je, ni mambo gani napaswa kuzingatia wakati wa kuandaa wa Wasifu binafsi (CV)? i. Juu Kabisa Mhusika ataje majina yote rasmi anayotumia kwa herufi kubwa kama yalivyo kwenye vyeti au viapo kama vipo. ii. Maelezo yake kwa kifupi Matarajio yake na ofisi anayoombea kazi itegemee nini toka kwake. iii. Historia yake ikiwemo;- Miaka yake Jinsia yake Hali ya ndoa Uraia iv. Historia ya Elimu Aeleze elimu aliyonayo kuanzia kiwango kikubwa cha elimu alichonacho hadi cha mwisho cha chini alichoanzia ikiwemo, Vyuo alivyosoma na mwaka aliohitimu na vyeti alivyotunukiwa kwa mfano: Masters of Science in Human Resource Management – Mzumbe University 2015, Bach...